*Kusajili watahiniwa wa Mitihani ya ndani na nje (Internal & External exams) kwenye mfumo* Wakuu/makamu/Wataaluma kupitia akaunti zao wanaweza kusajili watahiniwa (Candidates). Baada ya kusajili jina au aina ya mtihani, atasajili watahiniwa sasa kwa kubofya; `Academics=>Exams=>bofya button ya View/jicho ya mtihani husika=> Registered Candidates (Chagua darasa moja moja e.g. Class I/Form I)=>Register Candidates=> Select candidates to register (Chagua watahiniwa wa kusajili) kwa kutick=> Register.` Baada ya ku-register, mfumo unachakata automatically namba za mitihani za watahiniwa wote na kwa hatua hii, kwa sasa wataaluma/wakuu wanaweza kupakua CAL (collective attendance list) ya wanafunzi wote wa darasa husika waliosajiliwa kwa mtihani huo kwa kubofya `Exams=>View Exam=>Registered Candidates=>Download CAL`. Hiyo CAL itaonesha wanafunzi wote waliosajiliwa kwa kila somo, idadi ya masomo kwa kila mwanafunzi aliyosajiliwa kusoma kwa shuleni. *NB:* alama ya dash (-) inaonesha, mwanafunzi husika amesajiliwa kusoma somo husika. *Angalizo;* Kwa wanafunzi waliosajiliwa kwenye mfumo kusoma masomo na unauhakika kuwa kwa mtihani huu, hawatashiriki kwa changamoto mbalimbali, hivyo wasisajiliwe kufanya mtihani ili kuepuka kuwa na orodha ndefu ya wanafunzi ambayo wengine ni watoro wa mda mrefu. Pia, kwa kuwa function ya kusajili watahiniwa itakuwa inategemea 100% wanafunzi waliosajiliwa kwenye mfumo na wanaosoma masomo husika.
